Mawakibu za watu wa Karbala zinaomboleza kifo cha balozi wa Imamu Hussein (a.s) Muslim bun Aqiil na watoto wake wawili

Maoni katika picha
Pamoja na kuuwawa kwa balozi wa harakati ya Imamu Hussein (a.s) Muslim bun Aqiil mwezi tisa Dhulhijja, lakini imekua desturi ya waombolezaji wa Ashura kizazi na kizazi kuifanya siku na nne katika mwezi wa Muharam kua siku ya kumkumbuka mtukufu huyo, kama sehemu ya kumuenzi (a.s) hakika anastahiki zaidi ya hivyo, alijitolea nafsi yake kwa ajili ya kulinda Dini ya Mwenyezi Mungu na kumnusuru Imamu Hussein (a.s), habari ya kifo chake ilipo fika kwa Imamu alitokwa machozi na akasema: (Mwenyezi Mungu amrehemu Muslim amekwenda katika radhi na pepo ya Mwenyezi Mungu, tambueni hakika yeye amemaliza wajibu wake na umebaki wajibu wetu).

Huo ni muendelezo wa kumuomboleza Abu Abdillahi Hussein (a.s) aliye tokwa na machozi kwa kifo chake, mawakibu za watu wa Karbala zimeomboleza msiba huu huku mazingira yao yakisema: kama macho yako yalitoka machozi ukiwa peke yake ewe kiongozi wetu mwaka wa 60 hijiriyya, sisi wapenzi na wafuasi wako tunalia kwa kilio chako machozi ya damu.

Mawakibu za waombolezaji za watu wa Karbala zilizo kuja katika malalo mawili tukufu, ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), zimekumbuka ushujaa na msimamo wa balozi wa Imamu Hussei Muslim bun Aqiil (a.s), pamoja na watoto wake walio uwawa Muhammad Asghar na Ibrahim.

Fahamu kuwa ni desturi ya waombolezaji wa Ashura siku kumi za mwanzo kila moja imepangiwa mtu maalum katika kuelezea msiba huo mkubwa mbinguni na ardhini, utaratibu huo umekua ukifanywa karne na karne, usiku wa mwezi nne na mchana wake umepangwa kuzungumzia kifo cha balozi wa Imamu Hussein Muslim bun Aqiil (a.s) shahidi wa kwanza katika harakati ya Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: