Kwa mwaka wa pili mfululizo na kwa kuhudhuria na kushiriki ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu: Tuuz Khurumato yapandisha bendera ya kuomboleza msiba wa Imamu Hussein…

Maoni katika picha
Mwaka wa pili mfululizo kutokana na mapenzi ya watu wa Tuuz Khurmato katika mkoa wa Swalahu Dini, umewasili ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu ukiongozwa na mkuu wa idara ya Tablighi kwenye kitengo cha Dini Sayyid Muhammad Mussawi katika shughuli ya kupandisha bendera ya huzuni na kuomboleza Ashura, katika moja ya viwanja vya Umma katika mji huo, na kuhudhuriwa na mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu wa mji huo pamoja na wawakilishi wa vyombo vya ulinzi na usalama na wakazi wa mji huo.

Sayyid Mussawi amesema kua: “Hakika ni jambo zuri kushirikiana na wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika huzuni za kuomboleza kifo cha Abul-Ahraar Imamu Hussein (a.s), huu ni mwaka wa pili mfululizo Atabatu Abbasiyya inashiriki katika shughuli hizi ambazo zimekua zikifanywa na watu wa mji huu, walio simama imara dhidi ya magaidi wa Daesh na wakajitolea mashahidi wengi na majeruhi walio jifunza ushujaa kutoka kwa bwana wa Mashahidi (a.s)”.

Akaongeza kua: “Shughuli hiyo ilikua na athari kubwa katika nafsi za wahudhuriaji na watu wa mji huo kwa ujumla, hakika bendera hiyo inamaana kubwa kwao”.

Fahamu kua shughuli ya kupandisha bendera ya huzuni na maombolezi ya Husseiniyya ni jambo linalo fanywa ndani na nje ya Iraq kama sehemu ya kutangaza kuanza kwa msimu wa huzuni za Husseiniyya na kuingia mwezi mtukufu wa Muharam.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: