Baada ya mke wa Abdullahi Alkalbiy kujiunga na jeshi la Imamu Hussein (a.s), Ummu Wahabi aliomba kujiunga naye ilia pate shahada, bwana wa mashahidi (a.s) akamwambia: (Mmelipwa kheri kutokana na Ahlulbait, rudu ukakae kwa wanawake Mwenyezi Mungu akurehemu, hakika wanawake hawapigani), akarudi kukaa na wanawake wenzake, lakini akapata shahada baada ya kuuwawa mume wake Abullahi.
Abdullahi bun Umair Alkalbiy na mke wake Ummu Wahabi (r.a) walikua wanamuhami Abu Abdillahi Hussein (a.s), Abdullahi bun Umair Alkalbiy aliuwawa mbele ya Imamu Hussein (a.s), aliomba ruhusa ya kwenda kupigana na jeshi la Omari bun Saadi kwa bwana wa mashahidi (a.s) akapigana kwa ujasiri mkubwa kwa ajili ya kumlinda Imamu wa zama zake hadi akapata shahada.
Hiyo ndio kawaida ya wafuasi wote wa Imamu Hussein katika kila zama, wao huwa wakwanza kulinda misingi yao na miji yao, njia ya Hussein (a.s) hufatwa na majemedari.