(Hakika mimi sitambui wafuasi bora na waaminifu kushinda wafuasi wangu).. wafuasi wa Imamu Hussein (a.s) wamedhuria katika msimu wa maombolezo ya Ashura…

Maoni katika picha
Mawakibu za kuomboleza za watu wa Karbala –Ni desturi ya waombolezaji wa Husseiniyya kwa karne na karne-, usiku na mchana wa mwezi tano Muharam humzungumzia Habibu bun Mudhwahiri Asadiy (r.a), husomwa mashairi na kaswida pamoja na kupigwa ngoma za mawakibu kwa kukumbuka msimamo wa haki aliokua nao.

Toka alasiri ya Alkhamisi Muharam tano sawa na (5 Septemba 2019m) mawakibu za zainjiil na matam zimeanza kuadhimisha kumbukumbu yake hadi katikati ya usiku, chini ya uangalizi wa vitengo vya utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu ambayo hua ni kituo cha kwanza cha mawakibu hizo.

Rais wa kitengo cha mawakibu na maadhimisho ya Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu bwana Riyadh Ni’mah Salmaan, ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika kuwakumbuka wafuasi wa Imamu Hussein (a.s) akiwemo Habibu bun Mudhwahir Asadiy kupitia mawakibu za waombolezaji wa Karbala, ni sehemu ya kuwaenzi watu hao watukufu kwa jinsi walivyo jitolea katika kumnusuru Imamu Hussein na watu wa nyumbani wake (a.s), jambo hili limekua likifanywa kizazi kwa kizazi hurudiwa kila mwaka”.

Akamaliza kwa kusema: “Watumishi wa kitengo cha mawakibu na maadhimisho ya Husseiniyya pamoja na wale wa kujitolea kutoka vitengo vingine wanafanya kila wawezalo kuongoza mawakibu hizo kuanzia mwanzo wa matembezi yao hadi mwisho na kuhakikisha hazitatizi harakati za mazuwaru watukufu”.

Kumbuka kua Mawakibu za kuomboleza ndani ya siku (13) za kwanza katika mwezi wa Muharam ni za watu wa Karbala, jambo hilo ni mazowea yaliyo dumu kwa kwa miaka mingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: