Hussein alimwambia Saidi bun Abdillahi Alhanafiy.. (Utakua mbele yangu peponi)

Maoni katika picha
Kujitolea na msimamo hadi hatua ya mwisho ndio mwenengo halisi wa wapenzi wa Imamu Hussein na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kwa karne na karne, wamethibitisha kua wako tayali kujitolea nafsi zao kwa ajili ya kunusuru Dini na kutetea haki pamoja na kumnusuru Imamu Hussein (a.s), aliye uwawa kwa ajili ya kuonyesha njia kwa kila anayetaka kufuata mwenendo wake baada yake.

Na huo ndio msimamo wa Saidi bun Abdullahi Alhanafiy (r.a) alisimama mbele ya Imamu Hussein (a.s) katika swala ili amlinde na mishale ya maadui, alichomwa mishale hadi ikajaa mwili mzima akaanguka chini, akamuangalia Imamu Hussein (a.s) kisha akasema: (Nimetekeleza ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akamwambia (a.s): (Ndio, utakua mbele yangu peponi).

Kujitolea kwa wafuasi wa Imamu Hussein (a.s) hakujaisha hadi leo, bado wanaendelea kujitolea kwa hali na mali ukiwa ni mwendelezo wa kuenzi msimamo wa Saidi bun Abdullahi Alhanafiy (r.a) kwa ajili ya kulinda taifa na maeneo matukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: