Ilitokea siku kama leo mwezi sita Muharam 61 hijiriyya: Jeshi lilikusanyika katika ardhi ya Karbala kwa ajili ya kumshambulia Imamu Hussein (a.s) na Habibu bun Mudhwahir alikwenda kuwaomba watoto wa Ammi zake waende kumnusuru Imamu Hussein (a.s)…

Maoni katika picha
Siku ya mwezi sita Muharam mwaka 61h, jeshi lilikusanyika katika ardhi ya Karbala chini ya kamanda mkuu Omari bun Saadi (laana iwe juu yake) kwa ajili ya kumshambulia Imamu Hussein (a.s), walikua elfu thelethini kwa mujibu wa riwaya.

Mwezi sita Muharam pia ni siku ambayo Habibu bun Mudhwahir aliwaomba bani Asadi waende kumnusuru Imamu Hussein (a.s), alimfuata Imamu (a.s) akamuambia: Ewe mtoto wa Mtume hapa karibu yetu kuna mtaa wa bani Asadi, unaniruhusu niende kuwaomba waje kukunusuru? Huenda Mwenyezi Mungu anaweza kutulinda kupitia wao, akasema: (Nimekuruhusu). Habibu kawafuata katikati ya usiku huku anajificha maadui wasimuone, akawaambia: Nimekuja kuwaambia habari njema, nimekuja kuwaomba mwende kumnusuru mtoto wa binti wa Mtume wenu.. Omari bun Saadi amemzunguka na jeshi kake, nyie ni watu wa familia yangu.. akajitokeza mtu mmoja katika bani Asadi anaitwa Abdullahi bun Bishri akasema: mimi wa kwanza kuitikia wito huo..

Wakaendelea kujitokeza watu wengine hadi wakafika watu tisini, wakatoka kwenda kumnusuru Imamu Hussein (a.s), akatoka mtu mmoja katika wanafiki akaenda kwa Omari bun Saadi akamuambia habari hiyo, Omari akamwita mmoja katika askari wake aitwae Azraq, akampa wanajeshi wapanda farasi mia nne akawaambia wawafuate bani Asadi.. bani Asadi wakatambua njama hiyo na wakajua kua hawawezi kukabiliana na jeshi hilo wakakimbia kwa watu wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: