Kwa picha katika malalo yake tukufu: Waombolezaji wa Ashura wanakumbuka ushujaa wa Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Imekua desturi ya wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) hususan hapa Iraq makao makuu ya kumuomboleza Imamu Hussein (a.s), hutenga siku miongoni mwa siku kumi za kwanza katika mwezi wa Muharam kwa ajili ya kumzungumzia mtu mmoja miongoni mwa watu muhimu waliokuwepo katika vita ya Karbala, ikiwa kama sehemu ya kuelezea zaidi msiba wa bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein (a.s), msiba unao ombolezwa mbinguni na ardhini, japokua vita ilipiganywa siku moja, bali nusu ya mchana wa mwezi kumi Muharam mwaka wa 61h.

Usiku na mchana wa mwezi saba Muharam umetengwa kwa ajili ya kumzungumzia Abulfadhil Abbasi (a.s), kutokana na kilicho tajwa katika riwaya kua siku ya mwezi saba Muharam mwaka wa (61h), Abulfadhil Abbasi (a.s) na baadhi ya wafuasi wa Imamu Hussein (a.s) walipewa jukumu la kwenda katika mto wa Furat na kupambana na maadui kwa ajili ya kumletea maji Imamu Hussein (a.s) na watu wake waliopo katika mahema, wakachukua viriba ishirini (20) na wakavijaza maji ya kunywa kwa ajili ya kuwasaidia na kiu kali waliyo kua nayo.

Kutokana na tukio hilo mawakibu za kuomboleza huongelea zaidi ushujaa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) katika vita ya Karbala na kujitolea kwake kumlinda nduku yake Imamu Hussein (a.s), pamoja na namna alivyo jizuwia kunywa maji akiwa katika mto wa Alqami kwa kukumbuka kiu cha ndugu yake.

Alikua na ushujaa wa baba yake Haidari (a.s) na alipambana vikali kumnusuru Imamu wa zama zake Abu Abdillahi Hussein (a.s) katika vita ya Twafu, yenye mafunzo mengi na mazingatio, kubwa likiwa ni uaminifu na kujitolea.

Kumbuka kua mawakibu za waombolezaji na watoa huduma ndani ya siku (13) za mwanzo wa mwezi wa Muharam, zinazo shiriki katika ziara ya Ashura ni za watu wa mkoa wa Karbala, huu ni utamaduni wa miaka mingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: