Hussein aliwaambia vijana wawili: (Mwenyezi Mungu awalipe kheri enyi watoto wa ndugu yangu kwa kuwepo kwenu na kuniliwaza…)

Maoni katika picha
Hakuna jambo kubwa kama kukutana waumini wawili kwa ajili ya kumnusuru Imamu wa zama zao, hadi wakauwawa mbele yake kishahidi na kupata utukufu wa kumuhami mjukuu wa Mtume (s.a.w.w), wakaacha majina yao katika ukurasa wa mashahidi watukufu.

Katika msafara wa bwana wa mashahidi (a.s) kulikua na vijana wawili, ambao ni Sefu bun Harithi bun Sariíy Aljaabiriy na Maliki bun Abdu bun Sariíy Aljaabiriy watoto wa baba mkubwa na mdogo, walibaki na Imamu hadi alipo zungukwa na maadui, Imamu akawaambia: (Enyi watoto wa ndugu yangu Mwenyezi Mungu atakulipeni malipo bora Zaidi kwa kuwa pamoja na mimi na kuniliwaza).

Waumini wangapi walio kutanishwa na haki, wakashikamana kwa ajili ya kunusuru Dini ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kunusuru misingi ya mjukuu wake baba wa watu huru (Abul-Ahraar) (a.s), hadi leo bado wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wanakutana katika kulinda maeneo matakatifu kutokana na mafundisho wanayo pata kwa wafuasi wa Hussein (a.s) katika vita ya Twafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: