Hussein aliwaambia: Ewe Qassim (Huzuni iliyoje kwa Ammi yako unamuomba anashindwa kukujibu, au anakupa jibu lisilo kusaidia, au anatoa msaada usio kufaa…)

Maoni katika picha
Ni Qassim mtoto wa Hassan Almujtaba (a.s) kipenzi wa mjukuu wa Mtume (s.a.w.w), alikua miongoni mwa vijana wa Twafu walio pambana vikali kwa ajili ya kumlinda Imamu Hussein (a.s), maneno ya bwana wa mashahidi kuhusu yeye yanaonyesha nafasi kubwa aliyo kuwa nayo katika moyo wake.

Alisema (a.s) siku aliyo uwawa Qassim (a.s): (Huzuni iliyoje kwa Ammi yako unamuomba anashindwa kukujibu, au anakupa jibu lisilo kusaidia, au anatoa msaada usio kufaa, wawe mbali watu walio kuua, ole wake aliye kuua).

Bado wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wanakumbuka ushujaa, kujitolea na msimamo wa Qassim (a.s) na wafuasi wengine wa Imamu (a.s) katika vita ya Twafu, ambayo imeendelea kua kilele cha kujitolea na shahada ndio alama kubwa ya wafuasi wa baba wa watu huru (a.s) katika kila zama na sehemu, vijana wa kiislamu bado wanafuata nyayo za Qassim bun Hassan (a.s) wakiiga ushujaa wake katika kulinda Dini na maeneo matakatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: