Miongoni mwa harakati maalum za mwezi wa Muharam, Maahadi ya Quráni tukufu/ tawi la Baabil chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imeweka kikao cha usomaji wa Quráni na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya wakazi wa mji huo.
Kikao hicho kimehusisha ujumbe kutoka kwa kiongozi wa tawi la Maahadi katika mji wa Baabil Sayyid Muntadhwar Mashaikhiy, ametangaza ratiba ya Maahadi katika msimu wa huzuni ndani ya mwezi wa Muharam na Safar, akafafanua kua: “Mapinduzi ya Imamu Hussein (a.s) yalikua ya kivita na kifikra, kwa hiyo Maahadi itakua na ratiba ya mawaidha ya kujenga fikra, Quráni na utamaduni katika vitongoji tofauti, pamoja na katikati ya mji, sambamba na kufundisha usomaji sahihi wa Quráni kwa mazuwaru ambao ndio walengwa wakuu wa ratiba hii, mwaka huu ni tofauti na miaka ya nyuma, kila kituo kitakua na walimu wasio pungua kumi na tano, ratiba hii inahusisha vituo vya usomaji wa Quráni vilivyopo katika barabara zinazo tumiwa na mazuwaru”.
Kumbuka kua Maahadi ya Quráni tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inamchango mkubwa wa kurekebisha usomaji wa Quráni kwa maefu ya mazuwaru, wanaokuja Karbala katika mwezi wa Muharam na Safar kupitia miradi ya ufundishaji wa kusoma Quráni kwa ufasaha.