Hussein alimuambia: Ali Akbaru (Mwenyezi Mungu akulipe kheri kwa malipo ya mtoto kwa mzazi wake)

Maoni katika picha
Anafanana na Mtume maumbile, tabia na kuongea, naye ni Ali Akbaru (a.s) aliyekua miongoni mwa watu watukufu walio uwawa Karbala, na miongoni mwa walio mliwaza bwana wa mashahidi (a.s) na wakapigana kumlinda, sio kwa kua ni baba bali ni Imamu wa zama zake.

Alikua na nafasi kubwa sana kwa Imamu Hussein (a.s), alipo toka kwenda kupigana Imamu (a.s) alisema: (Ewe Mola shuhudia watu hawa wanapigana na mtu anaye fanana sana na Mtume (s.a.w.w) maumbile, tabia na kuongea), pia akamuambia: (Mwenyezi Mungu akulipe kheri kwa malipo ya mtoto kwa mzazi wake).

Kwa nini Ali Akbaru (a.s) asiwe na utukufu mkubwa wakati ni mjukuu wa bwana wa waarabu Mustwafa na Murtadha (a.s) na bibi yake ni Fatuma Batuli (a.s), kijana huyu wa kihashim aliuwawa akiwa anamuhami baba yake bwana wa mashahidi (a.s), jina lake limeandikwa kwa nuru katika kurasa za historia.

Alikua na ataendelea kua kiigizo kwa kila kijana mfuasi wa madrasa ya Ahlulbait (a.s) katika kulinda Dini na maeneo matakatifu pamoja na kutetea haki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: