Upande wa Kibla ya watu huru na kujitolea Karbala tukufu: watoto wa Ali wanawapa pole watoto wa Imamu Hussein (a.s) katika kukumbuka kifo chake

Maoni katika picha
Waombolezaji wa Ashura wanaendelea kumiminika katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya usiku wa mwezi kumi Muharam, ikiwemo maukibu kutoka katika mji wa kiongozi wa waumini (a.s), maukibu ya watu wa Najafu Ashrafu waliokuja kuomboleza msiba huu.

Maukibu hiyo imehusisha watu wengi wa Najafu, walianza matembezi karibu na muda wa Maghribaini, katika barabara ya Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na wakaelekea upande wa malalo ya mbeba bendera ya Twafu na kamanda wa jeshi la Imamu Hussein (a.s), matembezi hayo yakaishia katika malalo ya bwana wa mashahidi baba wa watu huru Abu Abdillahi Hussein (a.s), waombolezaji walikua wamepandisha bendera za kuashiria msiba wa Imamu Hussein katika ardhi ya Karbala, ardhi ya kujitolea, kaswida za maombolezo na huzuni zimesikika pamoja na sauti za kumpa mole Imamu wa zama (a.f).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: