Maombolezo ya mauwaji wa Karbala yanasifa mbili kubwa ambazo ni sehemu na muda, haiwezekani kubadilisha utaratibu wake, siku kumi za kwanza katika mwezi wa Muharam zitaendelea kua siku za kuomboleza na huzuni, kuanzia siku ya kwanza huendelea kuongezeka huzuni hadi siku ya tisa na kilele chake huwa siku ya kumi, mwezi tisa Muharam ni siku ambayo watu wema walijiandaa kuuwawa kwa ajili ya kutetea uhuru na kulinda Dini.
Kwa hiyo utakuta makundi ya waombolezaji waliokuja katika mji wa shahada na kujitolea, mji mtukufu wa Karbala wanaishi katika majonzi makubwa kutokana na msiba huo, wakielekea usiku wa mwezi kumi, usiku wa kuagana wapendanao, usiku huo bwana wa mashahidi alikesha akiangalia hema zake huku akijua kitakacho mtokea yeye na watu wa nyumbani kwake pamoja na wafuasi wake siku inayo fuata.
Kama kawaida katika usiku huu watu hufurika katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya na kwenye eneo la katikati yake, hukesha wakiswali na kuomba dua kama alivyo fanya Imamu Hussein (a.s) na wafuasi wake, sauti zao husikika kama sauti za nyuki.