Katika juhudi za kupata picha katikati ya matukio: Kituo cha uzalishaji Alkafeel na matangazo mubashara kimefunga zaidi ya kamera 55

Maoni katika picha
Tangu siku ya mwezi mosi Muharam, kama kawaida katika kila msimu wa maombolezo, watumishi wa kituo cha uzalishaji Alkafeel na matangazo mubashara chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, wamefanya kazi kubwa ya kuhakikisha wanapata picha nzuri katikati ya matukio ya waombolezaji na watoa huduma, pamoja na kufikisha sauti ya waombolezaji kila sehemu ya dunia, sambamba na harakati za Ataba tukufu katika kutoa huduma, kwa kufunga zaidi ya kamera (55) ndani na nje ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na kwenye eneo la katikati ya Ataba hizo.

Jambo hilo lipo katika mkakati wa Ataba kwenye sekta ya habari, wamejitahidi kwa kiasi kikubwa sana.

Mkuu wa kituo hicho Ustadh Bashiri Taajir ametuambia kuhusu mkakati maalum wa kurusha habari za Ashura kua: “Kituo kimeweka mikakati madhubuti ya upigaji wa picha, watumishi wana uwezo na uzowefu mkubwa katika swala hilo, wanapiga picha zenye ubora mkubwa zinazo faa kurushwa na makumi ya vyombo vya habari ndani na nje ya Iraq, wamefanikiwa kurusha matukio haya katika mji wa Karbala”.

Akaongeza kua: “Tunafanya kazi kila siku ndani ya mwaka mzima lakini katika siku za ziara maalum na matukio ya kidini kazi zetu huongezeka, kama ilivyo katika maombolezo ya Ashura, tumeandaa mkakati utakao tusaidia kurusha kila kitu katika maombolezo haya ndani ya Ataba mbili na kwenye eneo la katika ya Ataba hizo, tunafanya kazi saa ishirini na nne, tumeandaa masafa maalum kwa chombo chochote cha habari kitakacho taka kurusha matangazo yenye ubora (Clean) watumie anuani ifuatayo:

E3B at 3°E
Down:11579.4 H
SR:3200
Mod: DVBS28PSK
FEC:3/4
HD/MPEH-4
Akafafanua kua: Unaweza kufuatilia matangazo haya kupitia link ya matangazo mubashara katika Yuotube: https://www.youtube.com/channel/UCy0MMgRho_O8jxiIj46qMxw

Au matangazo mubashara kupitia facebook:

https://m.facebook.com/alkafeel.for.artistic.production/
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: