Rais wa kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya: Jumla ya maukibu na vikundi vya kutoa huduma (624) wameshiriki katika ziara ya Ashura

Maoni katika picha
Rais wa kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya bwana Riyadh Ni’mah Salmaan amesema kua: Idadi ya mawakibu zilizo shiriki katika ziara ya Ashura na zilizo sajiliwa rasmi mwaka huu wa (1441h) zimefika (624) maukibu zote ni za watu wa Karbala, kwani siku hizi ni maalim kwa watu hao.

Akasisitiza kua: “Hii ndio orodha ya Mawakibu zilizopo ndani ya mkoa wa Karbala, ukitoa Mawakibu ambazo hazikusajiliwa na huduma zinazo tolewa na watu wanaokuja kutoka mikoa mingine.

Akaongeza kua: “Kuna maukibu (200) za zanjiil na matam zinafanya shughuli za kuomboleza, na maukibu (424) zinafanya shughuli ya kuhudumia mazuwaru kwa kuwapa chakula na vinywaji pamoja na kuwapatia sehemu za kupumzika na malazi na huduma zingine tofauti, kuna maukibu zingine zina kua na kitengo cha maombolezo pamoja na kitengo cha kutoa huduma, asilimia kubwa zitaendelea kuwepo hadi mwezi kumi na tatu Muharam, zikiendelea na kazi walizo anza kufanya tangu siku ya Muharam mosi”.

Akasema: “Kitengo kilifanya mikutano kadhaa na viongozi wa mawakibu hizo kabla ya kipindi cha Ashura, kwa ajili ya kuelekezana kanuni na utaratibu wa maombolezo haya na kupunguza changamoto mbalimbali kwa ajili ya kufikia lengo la kutoa huduma bora zaidi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: