Muhimu… kuanza kwa matembezi ya (Towareji) ya milele

Maoni katika picha
Baada ya swala ya Adhuhuri mwezi kumi Muharam (1441h) sawa na (10 Septemba 2019m) yameanza matembezi ya towareji.

Matembezi hayo yameanzia katika Qantwara ya Salam na kupitia katika barabara ya Jamhuriyya hadi kwenye Atabatu Husseiniyya kisha wakapita katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu na wakaishia kwenye Atabatu Abbasiyya, ulinzi uliimarishwa katika maeneo yote.

Matembezi ya Towareji ni maandamano ya amani kwa ajili ya kuomboleza maswaibu ya Husseiniyya, yanayo fanywa na watu wa Towareji (wilaya ya Hindiyya iliyopo katika mkoa wa Karbala umbali wa kilometa 20 kutoka makao makuu ya mkoa huo) yakiwa kama ishara ya kuitikia wito wa Imamu Hussein (a.s) siku ya mwezi kumi Muharam, ni moja ya sehemu ambayo hukusanyika idadi kubwa ya watu, ni tukio la aina yake la maombolezo ya Husseiniyya, yalianza mwaka (1303h) sawa na mwaka (1885).

Wazee wanahadithia kua mwezi kumi Muharam baada ya kumaliza kusoma maqtal (majlis) katika nyumba ya Sayyid Swalehe Qazwini lilitoka kundi kubwa la watu huku wakisema: (Waa Hussein… Waa Hussein) katika barabara za mji huo, miaka iliyo fuata wakawa wakitoka wanatembea kwenda Karbala siku ya mwezi kumi baada ya swala ya Adhuhuri kwa kuanzia katika Qantwara Salam, iliyopo umbali wa kilometa 5 hadi kwenye kaburi la Imamu Hussein (a.s) na matembezi hayo hutanguliwa na watu wa Towareji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: