Maalum kwa mtandao wa Alkafeel: Picha za matembezi ya Towareji ya kuomboleza

Maoni katika picha
Picha za matembezi ya Towareji ya kuomboleza yaliyo fanyika leo Jumanne mwezi kumi Muharam (1441h) sawa na (10 Sptemba 2019m) baada ya swala ya Adhuhuri, picha hizi zimepigwa na kituo cha uzalishaji Alkafeel na matangazo mubashara chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, walianza kupiga picha tangu mwanzo wa matembezi haya hadi mwisho ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakipitia malalo ya ndugu yake Imamu Hussein (a.s) na kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.

Fahamu kua matembezi ya Towareji yalianza kufanywa na watu wa Towareji katika wilaya ya Hindiyya mkoa wa Karbala umbali wa mlometa (20) kutoka mjini Karbala, kama sehemu ya kuitikia wito wa Imamu Hussein (a.s) siku ya mwezi mumi Muharam pale alipo sema: (Je! Kuna wa kuninusuru aje kuninusuru?), matembezi hayo ni miongoni mwa mikusanyiko mikubwa ya watu duniani, ni tukio la aina yake katika Dini, yalianza mwaka wa (1303h) sawa na mwaka (1885m).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: