Uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya watangaza kufanyika kisomo cha kuwarehemu mashahidi wa matembezi ya Towareji

Maoni katika picha
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mtukufu..

Uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya watangaza kufanyika kwa kisomo cha kuwarehemu mashahidi wa matembezi ya Towareji katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu siku ya Jumamosi (14 Muharam 1441h) sawa na (14 Septemba 2019m) kuanzia saa tisa hadi saa kumi na mbili alasiri.

Kisomo hicho kinategemea wapenzi wa bwana wa mashahidi (a.s) kushiriki katika kuziliwaza familia za mashahidi (r.a) na kumuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awaruzuku shifaa ya Imamu Hussein (a.s) siku ya kiyama hakika yeye ni mwingi wa kusikia mwingi wa kujibu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: