Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaendesha semina ya kuwajengea uwezo watumishi wa ofisi ya wahadhiri wa Husseiniyya katika idara ya wanawake itakayo dumu kwa muda wa siku kumi.
Mkufunzi wa semina hiyo bwana Abdullahi Ismaiil Nuuri ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tunafanya semina hii itakayo dumu kwa muda wa siku kumi kwa kusoma saa tatu kila siku, kwa lengo la kuongeza uwezo wa watumishi wa idara hiyo katika usanifu na uzalishaji”.
Akaongeza kua: “Katika wiki ya kwanza tumewafundisha mambo maalum ya msingi katika uandishi wa miradi kwa namna ambayo itawawezesha kupangilia miradi ambayo imesha kua tayali pamoja na kuandaa ratiba kitaalamu katika kazi zao”.
Kumbuka kua kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu huendesha semina mbalimbali za kujenga uwezo kwa watumishi wa idara na vitengo vyote vya Ataba, kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuwafanya waendane na maendeleo yaliyopo katika sekta zao.