Ilitokea siku kama ya leo mwezi kumi na mbili Muharam mwaka 61h: Kuwasili watu wa Imamu Hussein waliotekwa katika mji wa Kufa

Maoni katika picha
Mwezi kumi na Moja Muharam msafara wa Ahlulbait (a.s) waliotekwa ulianza safari ya kuelekea Kufa kwa kupitia njia ya jangwa, wakiwa na machungu makubwa ya kilicho wapata siku waliyokaa karibu na miili ya mashahidi.

Msafari uliwasili Kufa mwezi kumi na mbili Muharam mwaka (61h), watu wakufa wakashangaa na tutoka barabarani, wakawa wanauliza kwani baadhi yao walikua hawajui mateka hao ni wakina nani, huku wanao wajua wanatoka majiani wakiwa wanalia kwa uchungu.

Baada ya msafara wa mateka kuwasili Kufa ulikwenda moja kwa moja katika Qasri la utawala, wakiwa pamoja na kundi kubwa la watu wa kufa wanaolia kwa uchungu kutokana na matatizo wanayo pewa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), na mambo yaliyo fanywa na jamaa zao ikiwa ni pamoja na kuvunja ahadi kwa mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) na Imamu wa waislamu Hussein (a.s), na sasa watu wa nyumbani kwake wanawake kwa watoto wamekua mateka, na kichwa chake kinazungushwa katika mji wa Kufa kikiwa juu ya mkuki, wakati walimwita awe kiongozi wa umma wa waislamu.

Wakati wanatembea bibi Zainabu (a.s) aliongea kwa uchungu kutokana na kuondokewa na kaka yake na kutekwa kwa familia yake, aliwaangalia watu wa Kufa na akazungumza maneno makali nafasi haitoshi kuyaandika.

Kichwa cha Hussein (a.s) kikaingizwa katika Qasri la utawala, na kuwekwa mbele ya (maluuni) Ibun Ziyadi akawa anapiga kichwa kile kitukufu kwa fimbo yake akiwa amejaa furaha, kisha mateka ambao ni wanawake na watoto wakaingizwa kwa Ibun Ziyadi, Ibun Ziyadi akamwambia bibi Zainabu (a.s) kwa dharau na kejeli: (Alhamdulillahi Allah amekufedhehesheni na kukuuweni na kudhihirisha uongo wenu), bibi Zainabu (a.s) akamjibu kwa kujiamini: (Alhamdulillaahi Allah ambaye ametukirimu kwa Mtume wake Muhammad (s.a.w.w) na akatutakasa na uchafu, hakika waovu hufedheheshwa na wachafu hukadhibishwa na wala sio sisi).

Ibun Ziyadi akasema: Umeona Mwenyezi Mungu amewafanyaje watu wa nyumbani kwako?

Akasema (a.s): (Mwenyezi Mungu amewaandikia shahada na atawakusanya pamoja na wewe na mtahojiana mbele yake).

Kiasha Imamu Sajjaad (a.s) akasimama mele ya Ibun Ziyadi, Ibun Ziyadi akamuuliza: Nani wewe? Akamjibu: (Mimi ni Ali bun Hussein). Akasema: Mwenyezi Mungu hakumuua Ali bun Hussein? Akamjibu: (Nilikua na ndugu anaitwa Ali bun Hussein ameuliwa na watu). Ibun Zitadi akasema: Kauliwa na Mwenyezi Mungu. Imamu akamwambia: (Mwenyezi Mungu huchukua nafsi wakati wa kifo chake), Ibun Ziyadi akakasirishwa na majibu ya Sajjaad (a.s), akamwita mtesaji akamwambia, kata shingo lake. Shangazi yake bibi Zainabu (a.s) akamkubatia na akaongea kwa ukali: (Ewe Ibun Ziyadi yatosha kumwaga damu zetu, wallahi sitamuachina kama unamuua muuwe pamoja na mimi) akaacha kumuua.

Roho mbaya na chuki ya Ibun Ziyadi haikuishia hapo, siku ya pili kichwa cha Imamu Hussein (a.s) kilendelea kuzungushwa katika barabara za Kufa, kwa ajili ya kuwatisha watu wa mji huo. Fahamu kua harakati ya Imamu Hussein (a.s) ilipita katika hatua nyingi hadi kuuwawa kwake kishahidi na yaliyo endelea baada ya kuuwawa kwake, ikiwa ni pamoja na kuwasili kwa Ahlulbait (a.s) waliotekwa katika mji wa Kufa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: