Ilitokea siku kama ya leo mwezi kumi na tatu Muharam mwaka 61h: Kuzikwa mwili mtukufu wa Imamu Hussein (a.s) na wafuasi wake

Maoni katika picha
Baada ya Omari bun Saadi kuwapeleka watu wa nyumba ya Mtume (a.s) katika mji wa Kufa na kuwaacha wale ambao kiongozi wa waumini (a.s) amewasifu kua ni mabwana wa mashahidi duniani na akhera, wakiwa wamelala katika uso wa aridh wakipigwa jua na vumbi, akiwemo bwana wa vijana wa peponi, wakiwa wanaangaziwa na nuru ya Mwenyezi Mungu pamoja na kupuliziwa harufu nzuri.

Mwezi kumi na tatu Muharam Zainul-Aabidina (a.s) alikuja kumzika baba yake (a.s), kwa sababu Imamu Maasumu hazikwi ispokua na Imamu Maasum mfano wake.

Historia inatuambia kua, Sajjaad (a.s) aliwakuta bani Asadi wamesimama mbele ya maiti hizo, wakiwa wamechanganikiwa hawajui cha kufanya, hawajui maiti hii ya nani na ile ya nani kwa sababu zikiua zimekatwa vichwa, wanaulizana hawa ni wakina nani? Wanatokana na familia zipi? Alipo fika (a.s) akaanza kuwabainishia na kuwatajia majina yao, akawapambanulia bani Hashim na wasiokua bani Hashim, sauti za vilio zikaongezeka, huzuni ikawa kubwa sana kwa bani Asadi.

Kisha Imamu Zainul-Aabidina (a.s) akaufuata mwili wa baba yake, akaukumbatia na kulia sana, akaenda sehemu ya kaburi akatoa udongo kidogo, akakuta kaburi tayali limesha chimbwa, akamlaza kaburini huku anasema: (Bismillahi wa fii sabili llahi wa ala milatu Rasulu-Llahi, swadaqa Llahu wa Rasuluhu, maasha-allahu laa haula wala quwata illa billahil-adhiim), alimuweka kaburini peke yake bila kusaidiwa na bani Asadi, akawaambia (a.s): (Hakika ninao wanao nisaidia), baada ya kumlaza kaburini akaweka shavu lake katika shingo tukufu la baba yake akasema: (Bishara njema kwa ardhi inayo sitiri mwili wako mtakatifu, hakika dunia baada yako ni giza, na akhera imengáa kwa nuru yako, usiku umekua mrefu na huzuni itadumu, Mwenyezi Mungu awachagulie watu wa nyumbani kwako nyumba ambayo wewe umeenda kuishi, nakutakia Amani ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na rehma zake na baraka zake), akaandika juu ya kaburi: (Hili ni kaburi la Hussein bun Ali bun Abu Twalib aliye uwawa akiwa na kiu akiwa mdhulumiwa).

Kisha akafuata maiti ya Ammi yake Abbasi (a.s) akaikuta ikiwa katika hali mbaya sana ambayo iliwahuzunisha malaka wa mbinguni na akaliliwa na viumbe wa peponi, Imamu akasema: (Hakuna zuri duniani baada yako ewe mwezi wa bani Hashim, nakutakia Amani ewe shahidi mtukufu na rehma na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yako), akamchimbia kaburi na akamzika peke yake kama alivyo fanya kwa baba yake, akawaambia bani Asadi: (Ninao wanao nisaidia).

Ndio, akawaachia kazi Bani Asadi ya kuwazika mashahidi watukufu, akawaambia wachimbe kaburi mbili kubwa, ya kwanza wakazikwa bani Hashim na ya pili wakazikwa wafuasi wa Imamu.

Shahidi wa karibu zaidi na Imamu ni mwanaye mkubwa (a.s), Imamu Swadiq (a.s) anasema kumwambia Hamadi Baswariy: (Abu Abdillahi aliuwawa akiwa mgeni katika ardhi ya ugenini, analiliwa na wanaokwenda kumzuru na anahuzunikiwa na wasio kwenda kumzuru, wanaumizwa naye ambao hawakumshuhudia, kila anaye angalia kaburi la mwanaye anamrehemu, haki ilizuwiliwa, aliuliwa na watu waovu kisha wakamuweka jangwani aliwe na simba, walimzuwia kunywa maji ya mto Furat yaliyo kuwa yakinywewa na mbwa, wakapoteza haki ya Mtume (s.a.w.w) na wasia wake kwa watu wa nyumbani kwake, amekua karibu zaidi na wafuasi wake, upweke umempa wafuasi wengi na umbali baina yake na babu yake umemfanya kua karibu zaidi, hakuna anaye mfuata ispokua yule mwenye Imani ya kweli).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: