Katika tukio la kibinadamu linalo ongeza orodha ya misaada ya kibinadamu inayo tolewa na hospitali ya rufaa Alkafeel ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imeahidi kutoa matibabu bure kwa majeruhi wa matembezi ya Towariji, huku baadhi ya majeruhi hao wakiwa na hali mbaya, majeruhi wote wanatibiwa kutokana na hali zao huku kila mmoja akiwa chini ya uangalizi wa daktari bingwa.
Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa hospitali hiyo Dokta Jaasim Ibrahimi, akaongeza kua: “Hospitali ilipokea watu waliojeruhiwa katika matembezi ya Towariji, na baadhi yao wameruhusiwa baada ya kupata matibabu, na wengine bado wamelazwa wanaendelea na matibabu”.
Akasema: “Kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Husseiniyya tukufu Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai na waziri wa afya Dokta Alaa Alwani waliwatembelea wagonjwa walio lazwa hapa hospitali, na kukagua maendeleo yao, wakapongeza huduma wanazo pewa”.
Kumbuka kua hospitali ya rufaa Alkafeel ilishiriki katika ratiba ya kutoa huduma za afya kwa mazuwaru wa Ashura kwa kushirikiana na idara ya afya ya mkoa wa Karbala, na kutoa huduma za afya kwa mazuwaru wengi.