Atabatu Abbasiyya tukufu: Inaendelea na maombolezo katika siku ya mwezi kumi na tatu Muharam

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetangaza kuendelea na maombolezo katika siku ya mwezi kumi na tatu Muharam na kushuhudiwa mafuriko makubwa ya mazuwaru bila kutokea tatizo lolote.

Makundi ya mazuwaru yalianza kufanya matembezi kwa kutokea sehemu ambayo wamezowea kuanzia matembezi kila mwaka, eneo la (Sayyidah Juudah) karibu na makaburi ya zamani huku wakiimba kaswida za maombolezo.

Kisha wanapitia barabara ya Kibla ya Imamu Hussein (a.s) wanaenda hadi kwenye haram ya Abu Abdillahi Hussein (a.s), halafu wanapita katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu na kuishia katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Atabatu Abbasiyya tukufu imejipanga vizuri katika kutoa huduma na kuimarisha ulizi kutokana na ongezeko hilo la mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: