Hakika tutabaki katika ahadi: Maukibu ya taa za mbinguni wanaomboleza siku ya tatu ya Imamu Hussein (a.s) akiwa juu ya udongo wa Karbala

Maoni katika picha
Katika kukumbuka yaliyojiri mwezi kumi na tatu Muharam mwaka (61h), kama kawaida yao kwa mwaka wa sita mfululizo, jioni ya mwezi (13 Muharam 1441h) sawa na (13 Septemba 2019m) baada ya swala ya Isha, maukibu ya taa (kandili) za mbinguni inayo undwa na wafanyakazi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wakiwa pamoja na baadhi ya watoto, wote wamevaa nguo nyeupe na wamebeba mabango yaliyo andikwa majina ya mashahidi wa Twafu, kwa kuanzia jina la Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) kisha wafuasi wake watukufu.

Mawakibu hiyo hutanguliwa na wabeba bendera na misahafu, matembezi yao huanzia ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuelekea katika malalo ya bwana wa mashahidi (a.s) wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.

Huku wakikumbuka tukio la kuhuzunisha la mauwaji ya karbala, matembezi yameishia ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s) kwa kufanya majlis ya kuomboleza iliyo hudhuriwa na mazuwaru wengi, katika majlis hiyo zimesomwa tenzi na mashairi yanayo amsha hisia za huzuni na watu wamelia na kupiga vifua vyao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: