Mwezi kumi na tatu Muharam mji mtukufu wa Karbala umeshuhudia matembezi makubwa ya kuomboleza ambayo hufanywa na makabila ya kiarabu kila mwaka, kutoka katika vitongoji vya mkoa wa Karbala wakiwa wamepaka udongo nyuso zao kama sehemu ya kuonyesha huzuni zao, huku wamebeba vifaa vya kuzikia na bendera zinazo ashiria kuomboleza na wakijipiga vichwa na vifua, wanaenda katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) huku wakijikumbusha mazishi ya miili ya mashahidi wa siku ya Ashura walio uwawa katika vita ya Twafu.
Kutokana na maombolezo hayo idara ya wahadhiri wa kike katika Atabatu Abbasiyya tukufu hutumia nafasi hiyo kufanya majlis kubwa ya kuomboleza na matam ya mawakibu hiyo katika sardabu zote za haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kama sehemu ya kumpa pole bibi Zaharaa na bibi Zainabu (a.s), huratibu pia matembezi ya waombolezaji kwa kusaidiana na wakina dada wa Zainabiyyaat, kwa ajili ya kupangilia vizuri matembezi yao ndani ya haram tukufu.
Bibi Taghridi Tamimi makamo rais wa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: Idadi ya waombolezaji wa mwaka huu imekua kubwa sana tofauti na miaka ya nyuma, tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumefanya kila tuwezalo kuhakikisha matembezi yanafanyika kwa Amani na utulivu, ndani ya haram tukufu ya Abbasi tuliweka watu (40) kwa ajili ya kuelekeza watembeaji, na tulikua na wahadhiri (15) walio wekwa katika kila Sardabu kwa ajili ya kutoa mawaidha na kusoma kaswida za kuomboleza, zowezi limeisha salama bila tatizo lolote”.