Kuanzishwa ushirikiano mpya kati ya kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji na wizara ya ulinzi ya Iraq

Maoni katika picha
Ujumbe wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaa/26 Hashdi Shaábi) umemtembelea waziri wa ulinzi Sayyid Najaah Shimri kwenye makao makuu ya wizara katika mji mkuu wa Iraq Bagdad, miongoni mwa mambo muhimu waliyo kubaliana ni:

  • 1- Mheshimiwa waziri ameruhusu kutoa uongozi wa kikosi cha Nukhba kwa kamanda wa jeshi la Iraq aliye fanya kazi na kikosi cha Abasi tangu kuanzishwa kwake na akashiriki katika vita nyingi, ambaye jukumu lake kwa sasa ni afisa uhusiano kati ya uongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) na viongozi wa jeshi la Iraq, alikua na mchango mkubwa katika kulinda umma kwenye sekta mbalimbali.
  • 2- Mheshimiwa waziri ameonyesha heshima kubwa kwa wapiganaji wa Hashdi Shaábi amewapongeza sana wapiganaji walio jitolea kulinda taifa, wananchi na maeneo matukufu dhidi ya magaidi wa Daesh.
  • 3- Tunataraia kuona mchakato wa kuwa chini ya wizara ya ulinzi kwa baadhi ya vikosi vyake unakamilika ndani ya miezi miwili ijayo –Insha-Allah-.
  • 4- Wamekubaliana kuongeza kiwango cha ushirikiano baina ya Atabatu Abbasiyya na wizara, kwa ajili ya kufuatilia baadhi ya wapiganaji ambao taratibu za kustafu kwao zimechelewa kwa kuunda mkamati maalum ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • 5- Kikosi kinatarajia ushirikiano mzuri wa wizara utakao kiwezesha kuongeza wapiganaji kwa ajili ya kuimarisha ulinzi wa taifa dhidi ya maadui.
  • 6- Kikosi kimethibitisha kua kipo tayali kushirikiana na wizara kuboresha siraha za kivita na kuzifanya ziendane na mazingira ya sasa na ya baadae.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: