Program ya Al-Qamaru yahitimisha awamu ya kumi na saba likiwa na washiriki (45) kutoka mkoa wa Qadisiyya

Maoni katika picha
Program ya Al-Qamaru inayo simamiwa na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, imehitimisha mafunzo ya kumi na saba yaliyo kua na washiriki (45) kutoka mkoa wa Qadisiyya.

Program hii imeendeshwa na watu walio bobea kutoka Atabatu Abbasiyya, mafunzo yamefanywa kwa muda wa siku tatu ambazo imetolewa mihadhara ya mambo mbalimbali.

Ustadh Farasi Shimri ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Program hii katika awamu ya kumi na saba inayo lenga watu wa mkoa wa Qadisiyya, imetolewa mihadhara ya mada tofauti na walimu wenye uwezo mkubwa, wamezungumzia ukweli wa Dini pamoja na mambo ya kielimu na kijamii, hali kadhalika maswala ya mitandao na mtazamo wa sheria katika mambo hayo sambamba na usomaji wa kisasa”.

Akaongeza kua: “Washiriki wa mafunzo hayo wameushukuru sana uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwani katika mafunzo hayo wamepata mambo yanayo weza kuwasaidia kutatua changamoto katika jamii”.

Kumbuka kua kongamano la kitamaduni Al-Qamaru linalenga watu wa tabaka na umri tofauti, na kupambana na changamoto za kijamii pamoja na kuangalia namna ya kuzitatua kwa kutumia njia nzuri za kielimu wala sio njia za chuki na ugonvi, ambazo huwa na matokeo hasi na huleta madhara katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: