Alfajiri ya Jumatatu (16 Muharam 1441h) sawa na (16 Septemba 2019m) imeanza ratiba ya ushindi –hatua ya tano- kwa ushiriki wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaa/26 Hashdi Sha’abi).
Mkuu wa kikosi hicho Shekh Maitham Zaidi amesema kua: “Kikosi kilikuwa na majukumu kwenye opresheni ya Furaat-Uasat, upande wa miji ya Nakhibu kaskazini magharibi ya ziwa Razaza”.
Akaendelea kusema kua: “Kikosi cha Abbasi (a.s) kilikamilisha kazi zote kilizo pewa ndani ya muda uliopangwa”. Akabainisha kua: “Kazi walizo pewa ilikua ni kuimarisha ulinzi na kufanya msako jangwani, ili kumaliza mabaki ya Daesh katika eneo lenye ukubwa wa (mk 50)”, tulitembea umbali wa zaidi ya (km 17) bila kupata kitu chochote”.
Akaongeza kua: “Tulishirikiana na kikosi cha tisa cha deraya kutoka jeshi la serikali ya Iraq pamoja na vikosi vya usalama vya Karbala”, akasisitiza kua: “Kikosi kinashirikina na wapiganaji wa Nukhba na kikosi cha deraya pamoja na Liwaa ya Ummul-Banina”