Chuo kikuu cha Al-Ameed chasisitiza kua: Sisi tunafuata njia ya kutoa huduma katika mazingira salama kwa mazuwaru wa Karbala

Maoni katika picha
Katika ratiba ya hafla ya ufunguzi wa kongamano la kimataifa la kwanza kuhusu huduma za kitabibu kwenye ziara ya Arubainiyya, lililofanyika asubuhi ya Jumanne (16 Muharam 1441h) sawa na (16 Septemba 2019m) katika chuo kikuu cha Al-Ameed, chini ya kauli mbiu isemayo: (Huduma za matibabu ni nguzo ya amani kwenye ziara ya arubainiyya) kwa usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu pamoja na wizara ya afya, kulikua na ujumbe kutoka chuo kikuu cha Al-Ameed ulio wasilishwa na rais wa chuo hicho na rais wa kongamano Dokta Muayyad Ghazali, miongoni mwa aliyo sema ni: “Hakika siri ya kuendelea kwa umma na jamii ni kuwepo kwa nidhamu ya elimu malezi na utafiti, pamoja na kazi zinazofanywa na taasisi katika sekta ya elimu na tafiti, moja ya vitu muhimu katika maendeleo ya umma ni kufanya makongamano ya kielimu ambayo huwasilishwa tafiti zinazo elekeza namna ya kutatua changamoto zilizopo katika jamii, sambamba na kuazimia kufanyia kazi njia za kutatua changamoto na kupata matokeo tarajiwa, kutokana na mkakati wa kielimu”.

Akaongeza kua: “Leo tumekusanyika katika kongamano hili la (Kongamano la kwanza kimataifa la huduma za kitabibu katika ziara ya Arubainiyya), kwa ajili ya kujadili mazingira ya kutoa huduma za matibabu kwa mazuwaru, tunasisitiza kua tunafuata njia ya kutoa huduma katika mazingira tulivu kwenye ziara ya Karbala, huduma hizo zinahitaji kubaini tatizo na kuweka mazingira mazuri, na hayo ndio maelekezo ya Marjaa Dini mkuu kwani ni sehemu ya kulitumikia taifa na wanadamu”.

Akabainisha kua: “Ni muhimu kufanya makongamano ya aina hii kutokana na umuhimu wa huduma za matibabu kwa mazuwaru watukufu, jambo hili linahitaji kuweka mkakati maalum, na kuwa na mawasiliano ya karibu na uongozi wa Ataba mbili tukufu pamoja na taasisi za afya na wizara zingine zenye uhusiano na mambo ya afya, kisha kusimamia utekelezaji wa mkakati chini ya watalamu walio bobea na wenye uzowefu mkubwa wa mambo ya afya, kisha kuhakikisha vipengele vyote vilivyo elekezwa na wataalamu vinafanyiwa kazi”.

Akamaliza kwa kusema: “Bila hivyo haiwezekani kupata mafanikio yanayo kusudiwa na Marjaa Dini mkuu pamoja na muwakilishi wake kiongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kila mtu mwenye mapenzi na taifa hili anataka kuona mazingira ya upendo na amani kwa watu wa madhehebu zote kwenye ziara ya Arubainiyya”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: