Katika kufanyia kazi vipengele vya makubaliano kati ya chuo kikuu cha Basra na kituo cha faharasi na mpangilio wa maalumaat chini ya Maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wanafanya semina kuhusu taratibu za faharasi za kisasa na program ya (RDA) inayo tumiwa na maktaba ya kitivo cha adabu kwenye chuo kikuu pamoja na program ya (KOHA) inayo tumiwa na maktaba kubwa duniani kwa sasa.
Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kituo Ustadh Hasanain Mussawi: “Hii ni sehemu ya semina zinazo fanywa na kituo hiki kwa maktaba za serikali au binafsi, semina hii inatokana na makubaliano yaliyo fikiwa kati ya chuo kikuu cha Basra na Maktaba na Daru Makhtutwaat ya Ataba tukufu, moja ya kipengele cha makubaliano hayo ni kubadilishana uzowefu, jambo muhimu likiwa ni kuendesha semina za kitaalam, tumeamua kufanya semina hii kwa sababu watumishi wetu wana uzowefu mkubwa katika sekta ya faharasi na usanifu”.
Akaongeza kua: “Semina itafanyika kwa muda wa siku tano, itakua na sehemu mbili (nadhariyya na vitendo), katika utaratibu wa kubadilishana uzowefu katika sekta ya maktaba na faharasi, kwani watumishi wa kituo cha faharasi na mpangilio wa maalumaat katika Atabatu Abbasiyya wana ujuzi na uzowefu unao wawezesha kuendesha semina za aina hii katika viwango vyote”.
Washiriki wa semina wamesema kua: “Hakika semina ilikua nzuri na tumenufaika sana, tumefundishwa mambo yenye umuhimu mkubwa yanayo tufanya tuhisi kuingia kwenye ulimwengu mpya wa sekta hii, kulikua na mihadhara mizuri iliyo tuwezesha kuchota elimu ya kutosha, pamoja na masomo hayo tumepata fursa ya kuangalia Daru Makhtutwaat pamoja na idara ya tafiti, kwa ajili ya kupata baadhi ya taarifa zitakazo tusaidia katika kazi zetu”.