Miongoni mwa harakazi za kielimu zinazo lenga kufundisha utamaduni wa Quráni, Maahadi ya Quráni/ tawi la Hindiyya chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya semina maalum kwa walimu wanaofundisha usomaji wa Quráni na hifdhu, kundi kubwa la walimu linashiriki katika semina hii, ikiwa ni miongoni mwa juhudi za kuboresha kiwango cha elimu kwa wanafunzi.
Wanafundishwa hukumu za usomaji pamoja na njia za ufundishaji na mambo mengine, watafundishwa zaidi ya vipindi 30 vya masomo, semina imefunguliwa kwa ujumbe wa kiongozi wa Maahadi Sayyid Haamid Marábiy, amewahimiza walimu wanaoshiriki katika semina hii wajifunze kwa bidii ili wapate mafanikio bora kwa ajili ya kutengeneza kizazi kitakacho pambika na Quráni na kufuata muongozo wa vizito viwili kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi cha Mtume (s.a.w.w).
Fahamu kua Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya hufanya semina za masomo ya Quráni ndani ya mwaka mzima kwenye miji tofauti.