Katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s): Watu wa Karbala na maukibu zao za kuomboleza wanahuisha siku ya saba tangu kuuwawa kwa Imamu Hussein (a.s)

Maoni katika picha
Ni kawaida ya watu wa Karbala kufanya maombolezo kuanzia siku ya kwanza katika mwezi wa Muharam hadi siku ya kumi ambayo hua ni kilele cha maombolezo, halafu huomboleza tena siku ya kumi na tatu Muharam ambayo ni kumbukumbu ya kuzikwa kwa mashahidi wa Karbala, kisha huomoleza siku ya saba tangu kuuwawa kwa Imamu Hussein (a.s).

Maombolezo haya yamekua yakifanywa kizazi kwa kizazi na watu wa Karbala pamoja na mawakibu zao na mazuwaru watukufu, baada ya swala ya Isha mwezi kumi na saba Muharam 1441h yamefanyika matembezi ya kuomboleza kwa kuanzia ndani ya malalo ya Abu Abdillahi Hussein (a.s) na kuelekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) huku wakiimba kaswida za kuomboleza na kushika mishumaa kama ishara ya kumpa pole bibi Zainabu (a.s).

Walipo ingia katika haram tukufu wakafanya majlis ya kuomboleza iliyo ongozwa na mtoto wa marehem Shekh Haadi Karbalai, halafu akapanda mimbari Abdul-Amiir Umawiy na kuimba kuhusu maombolezo hayo, pia wakakumbukwa watumishi wa matembezi ya Husseiniyya pamoja na wahadhiri na washairi waliokua na mchango mkubwa katika kuhuisha maombolezo ya Husseiniyya.

Waombolezaji wa msiba huu wameweka mazingira ya huzuni kwa kila mshiriki, huku uhalisia wao unaonyesha kusema kua: “Kama wahakuhudhuria watu wa nyumbani kwako na wafuasi wako kwenye kaburi lako ewe Abu Abdillahi Hussein katika siku ya saba tangu kuuwawa kwako mwaka wa (61h), na wala haukuwashiwa mishumaa na kumwagiwa maji kaburi lako au kuombolezwa, hawa hapa wapenzi wako na wafuasi wako watu wa Karbala wamekuja kuomboleza na kumpa pole mama yako Zaharaa na babu yako Mtume (s.a.w.w), na kupoza moto wa msiba wako ambao hautapoa wala kuzimika kwa karne na karne”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: