Kikosi cha Abbasi kimekamilisha jukumu kililopewa katika opresheni ya Iraadatu-Nasru kwa kufanya ukaguzi katika eneo la zaidi ya 2km700

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganai (Liwaa 26 Hashdi Shaábi) kimemaliza jukumu kililopewa katika opresheni ya Iradatu-Nasru hatua ya tano.

Mkuu wa kikosi hicho Shekh Maitham Zaidi ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kua kikosi kimemaliza jukumu lake, kimefanikiwa kufanya ukaguzi eneo kubwa zaidi la jangwani linakadiriwa kuwa 2km700.

Akasema kua wapiganaji wetu hawajaona mabaki ya magaidi wa Daesh ndani ya eneo la umbali wa km50 kutoka katika kituo chake, akasisitiza kua kikosi kipo tayali kufanya kazi yeyote katika eneo wanalo simamia au eneo lolote ndani ya taifa letu kipenzi.

Fahamu kua kikosi kilianza kutekeleza jukumu walilo pewa katika opresheni ya Iradatu-Nasru hatua ya tano pamoja na kikosi cha Furaat Ausat kuanzia mji wa Nakhibu kuelekea kaskazini magharibi ya ziwa Razaza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: