Idara ya harakati katika kitengo cha malezi na elimu cha Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya warsha kwa watumishi wa shule za Al-Ameed chini ya anuani isemayo: (kupima viashiria na uchambuzi), warsha hii ni sehemu ya mafundisho endelevu yanayo tolewa na kitengo hicho kwa wafanyakazi,
Dokta Hassan Jadhili muwezeshaji wa warsha hiyo ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Lengo la warsha ya leo ni kuongeza uwezo wa walimu katika kupima viashiria na kuweka malengo ya kimkakati na kufuata utaratibu wa kuyafikia, pamoja na namna ya kufanyia kazi viashiria vya matokeo ya mwisho, katika warsha hii tumechambua mchakato wa kupima viashiria na umuhimu wake, sambamba na kuchagua utaratibu bora wa ufundishaji, baada ya kubaini lengo tumeweka mchakato mzuri wa kufikia lengo, baada ya kubaini mchakato tukaweka viashiria vya mafanikio au ubora kisha utaratibu wa kufanya tathmini, ambayo inaweza kufanywa kwa kutumia dodoso au njia nuyingine yeyote”.
Akaongeza kua: “Baada ya kuweka viashiria tulianza kuweka mbadala wake kisha tuka ainisha muda wa utekelezaji wake, na tukaweka utaratibu wa kushindanisha matokeo, lengo kubwa ni kuwa na ubora endelevu”.
Akamaliza kwa kusema kua: “Washiriki wa warsha hii wametoa ushirikiano mkubwa, ushirikiano huo umeonekana kupitia kazi walizo pewa na maswali yanayo ulizwa katika warsha”.