Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kufaulu kwa mkakati wake kwenye ziara ya Ashura

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kufaulu kwa mkakati wake kwenye ziara ya Ashura, kikasisitiza kua maelfu ya mazuwaru wamenufaika na mkakati huo, wakabainisha kua mkakati ulihusisha mambo yafuatayo:

  • - Kuweka vituo vya tabligh kwa ajili ya kujibu maswali kutoka kwa mazuwaru ndani na nje ya haram tukufu.
  • - Kugawa machapisho mbalimbali kwa mazuwaru.
  • - Kuswalisha swala za jamaa ndani ya haram, kwenye uwanja wa mlango wa Kibla na ndani ya sardabu pamoja na maeneo ya nje.
  • - Kujibu maswali ya watu wanaokuja kumzuru Abulfadhil Abbasi (a.s) ndani ya ofisi za kitengo hiki wakati wote.
  • - Kutoa mawaidha ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
  • - Kusambaza mubalighina katika mawakibu na Husseiniyyaat, kwa ajili ya kutoa muongozo na mawaidha ndani na nje ya mkoa wa Karbala.
  • - Kushiriki katika vipindi vya luninga na redio katika kujadili na kufafanua malengo ya ziara ya Ashura.
  • - Kuweka hadithi zinazo elezea utukufu wa ziara na malengo yake kwenye mabango ya ndani na nje ya haram tukufu.
  • - Kuweka mabango ya matangazo ya vitu muhimu anavyo weza kuvihitaji zaairu mtukufu ikiwa ni pamoja na mambo yanayo husiana na ziara na adabu zake.
  • - Kushirikiana na waombolezaji wa Towariji siku ya mwezi kumi na tatu Muharam.

Fahamu kua kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinauhusiano wa moja kwa moja na mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s), kwani kina jukumu la kumuandaa zaairu kiroho na kumfafanulia umuhimu na malengo ya ziara, ili kumfanya atambue malengo ya Imamu Hussein (a.s), ili kila mtu aweze kuchota maarifa ya namna ya kupambana na dhumla pamoja na matwaghuti kila sehem ya dunia, wala sio kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) peke yao, bali kwa waumini wa dini zote kwani hayo ndio mapinduzi ya Husseiniyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: