Bado kamati ya maandalizi ya kongamano la kimataifa kuhusu turathi za Karbala inaendelea kufanya vikao vyake, kongamano hilo litafanyika chini ya usimamizi wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu/ kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika kituo cha turathi za Karbala, chini ya kauli mbiu isemayo: (Turathi zetu ni utambulisho wetu) na anuani isemayo: (Nafasi ya turathi za Karbala katika maktaba za kiislamu) litakalo fanyika (7-8 Novemba 2019m) sawa na (10-11 Rabiul Awwal 1441h).
Vikao hivi ni kwa ajili ya kuhakikisha kongamano hilo linakua na matokeo mazuri, na kukagua utendaji wa kamati ndogo ndogo zinazo tokana na kamati kuu, na kuandaa mambo ya lazima katika kongamano hilo, sambamba na kujadili maandalizi kifedha na matangazo, pia wamekagua mada zitakazo wasilishwa, pamoja na kujadili watu muhimu wanaotakiwa kualikwa katika kushiriki kwenye kongamano na wageni waalikwa.
Wajumbe wa kikao hicho kitakacho fuatiwa na vikao vingine wamesisitiza kua, swala la turathi za Karbala lina umuhimu mkubwa, na wakahimiza kutumia vizuri muda ulio baki na kuhakikisha kongamano hilo linafanyika kama lilivyo pangwa.
Kumbuka kua kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, kimetoa wito kwa watafiti na wasomi washiriki katika kongamano hilo na kuandaa mada maalum.