Miongoni mwa mfululizo wa machapisho yake yanayo lenga kuongeza uwelewa wa waumini, kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa kitabu kiitwacho: (Maswali na majibu kuhusu maadhimisho ya Husseiniyya) kwa mujibu wa fatwa za Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Hussein Sistani na Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Muhammad Saidi Hakiim.
Kitabu hiki kimejadili mambo yanayo fanywa katika maadhimisho ya Husseiniyya kutokana na umuhimu wake wa kusambaza ujumbe wa Imamu Hussein (a.s) na mwenendo wake madhubuti, na namna uhai wa uislamu unavyo bakia kupitia mapinduzi ya Husseiniyya na kuenea kwake sehemu kubwa ya dunia, ilikua muhimu sana kufafanua maswala ya kisheria kuhusiana na maadhimisho hayo, kwa hiyo kitengo hiki kimefanya kazi ya kukusanya maswali yaliyo ulizwa kwa Maraajii hao wawili na kuyaweka kwenye kitabu ili kuwarahisishia wasomaji kusoma majibu kupitia kitabu hiki,
Kumbuka kua kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinajukumu la kujenga uwelewa kwa jamii katika mambo mbalimbali, na kufundisha uislamu sahihi kwa mujibu wa Quráni na kizazi kitakasifu.
Kutokana na umuhimu wa kitabu hiki kimesha chapishwa mara nyingi, pia kinapatikana katika kituo cha mauzo ya moja kwa moja kilicho chini ya kitengo cha Dini mkabala na mlango wa Imamu Hussein (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, unaweza kukisoma na kukipakua kupitia mtandao rasmi wa kitengo cha Dini kwenye link ifuatayo: https://alkafeel.net/religious/index.php?iss