Marjaa Dini mkuu kwenye khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya uwanja wa haram ya Imamu Hussein (a.s) leo (20 Muharam 1441h) sawa na (20 Septemba 2019m) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, amezungumza vipengele vingi vya kimaadili na kimalezi vinavyo gusa mazingira halisi tunayo ishi, akasisitiza zaidi umuhimu wa vijana kunufaika na nguvu zao katika kujenga umma, miongoni mwa aliyosema ni:
- - Vijana wana nguvu za akili na mwili zenye umuhimu mkubwa katika kila kazi.
- - Kujitambua kwa kijana ni muhimu sana.
- - Miongoni mwa mambo yatakayo mfanya kijana aonekane ni mtu muhimu ni kusoma katika umri huo.
- - Uwezo wa akili wa kijana unahitaji malezi maalum ili uweze kumnufaisha.
- - Lazima tujifundishe kutopoteza muda.
- - Mtu anatakiwa kuwa macho daima na kutoharibu muda.
- - Mwanadamu anatakiwa ajifunze na awe na malengo.
- - Wakati fulani mtu huchanganikiwa katika kupanga malendo na hushindwa kujua lenye manufaa na madhara kwake.
- - Wakati fulani mwanadamu anahitaji mtu wa kumuelekeza na kumuongoza.
- - Kijana atakapo jibidiisha katika masomo atafikia malengo.
- - Umri ni muhimu lakini mtu anaweza kuwa na uwezo mkubwa wa akili kushinda umri wake.
- - Kijana anaweza kukuza uwezo wa akili yake, hatakiwi kuwa mzembe, mvivu na kubweteka, akikua akili huwa makini.
- - Hakuna wakati ambao kijana hatakua mlengwa au utakosekana mlengo wa batili.
- - Kijana ndio mlekwa mkuu wakati wote.
- - Kijana anauzowefu mdogo ni rahisi kushawishika.
- - Kijana atakapokua makini na akawa na msimamo hawezi kutetereshwa na kitu chochote.
- - Katika vita ya Twafu vijana walikua na mtihani.
- - Historia haijaeleza kwa kina uhusiano wa Hussein (a.s) na Qassim (a.s), na uhusiano wake na mwanae Ali Akbaru au uhusiano wake na Abbasi pamoja na ndugu wa Abbasi.
- - Hatujaona sehemu inayo sema kua Qassim kutokana na kua na umri mdogo aliogopa au alitetemeka!! Au Ali Akbaru alikua anatamani kuendelea kuishi.
- - Vijana waliokua na Imamu Hussein (a.s) kila shaka aliwalea na akawafundisha kujitambua.
- - Hata kama kungekua na makumi ya vita kama ya Twafu zinsinge mteteresha Abulfadhil Abbasi (a.s) wala Ali Akbaru wala Qassim.
- - Vijana hao katika umri mdogo sio kwamba walimnusuru Imamu Hussein tu, bali wamekua kiigizo chema kwa waislamu wote.
- - Kijana anahitaji kuongozwa na Imamu Hussein (a.s) alikua kiongozi bora kwao.
- - Kwa kumnusuru kwao Imamu Hussein sio kwamba wamekua kiigizo cha vijana bali cha waumini wote na wamekua wakitajwa pamoja na bwana wa mashahidi (a.s).
- - Vijana waliokua na Imamu Hussein (a.s) wameacha historia ambayo kila mtu anajivunia ispokua mwenye matatizo ya akili.
- - Vijana hao hawakutoka pekeyao wala hawakufanya mambo bila muongozo, walitoka na Imamu Hussein (a.s) na walifuata maelekezo yake katika kila jambo.
- - Walikua na uchaguzi mgumu baina ya udhalili na kifo, wakakataa udhalili na kuchagua kifo na kwa hakika walishinda.
- - Vijana anapopata malezi mema na kitu muhimu ni kukua kwa akili anaweza kuwa na faida kubwa kushinda mtu wenye umri mkubwa.
- - Vita ya Twafu imejaa mafundisho, kila mwaka inapo somwa huwa sawa na inasomwa kwa mara ya kwanza, hupatikana mambo mapya hakika ni shule ya kudumu katika kila sekta.