Mwaka wa nne mfululizo: Jumuiya ya Skaut Alkafeel inafanya matembezi ya kuhuisha utiifu kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maoni katika picha
Baada ya Adhuhuri ya leo mwezi (20 Muharam 1441h) sawa na (20 Septemba 2019m) kwa mwaka wa nne mfululizo, jumuiya ya Skaut Alkafeel chini ya idara ya watoto na makuzi katika Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya matembezi ikiwa na washiriki zaidi ya (200) kutoka vitengo tofauti vya Skaut.

Matembezi yalianzia katika eneo la Baabu Bagdad kuelekea katika malalo ya Abul-Ahraar (a.s), kumpa pole Imamu wa zama Hujjat bun Hassan (a.f) na kuhuisha utiifu kwa bwana wa mashahidi (a.s), kisha wakaielekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu huku wakiwa wamebeba mabango yanayo ashiria maombolezo na kuimba kaswida za huzuni, miongoni mwa mabango waliyo kua nayo yapo yaliyokua yamechorwa yaliyo jiri katika vita ya Twafu pamoja na baadhi ya matukio ya majemedari wa Hashdi Shaábi.

Matembezi yalionyesha mazingira ya vita ya Karbala ya kujitolea na uaminifu sifa kubwa ya wafuasi wa Imamu Hussein (a.s), kama walivyo onyesha kujitolea kwa bwana wa maji mwezi wa bani Hashim kutitia igizo la mmoja wa wanaskaut, kisha matembezi yakaelekea katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na wakafanya majlis ndani ya haram hiyo tukufu, iliyo pambwa na usomaji wa Quráni tukufu na mashairi pamoja na matam.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: