Chini ya usimamizi wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu: Ujenzi wa jengo la vyoo litakalo saidia kuhudumia mazuwaru

Maoni katika picha
Kwa usimamizi wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu na kwa ihsani ya mfadhili, umeanza ujenzi wa jengo la vyoo liitwalo (Waahatu-Zaairu) litakalo saidia kutoa huduma mbalimbali, litasaidia kupunguza msongamano vyooni katika siku za ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, ukizingatia sehemu lililopo ambapo ni upande wa mlango wa Bagdad katika muelekeo wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hakuna jengo lolote la vyoo, baada ya kupata eneo linalo faa kujenga jengo la aina hiyo, ndipo ujenzi ukaanza na umesha piga hatua kubwa.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kua: “Mradi huu unatekelezwa kwa ajili ya kuhudumia mazuwaru wa malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), pia ni sehemu ya muendelezo wa miradi ya Atabatu Abbasiyya, ambapo ujenzi wa vyoo ni miongoni mwa miradi muhimu, mradi huu unafanywa chini ya usimamizi wa kitengo chetu na ufadhili wa mmoja wa wahisani, na watekelezaji ni moja ya mashirika ya ujenzi, limezingatiwa jambo la kutotatiza shughuli yoyote miongoni mwa shughuli za upanuzi katika Atabatu Abbasiyya siku za mbele”.

Miongoni mwa wasifu muhimu wa mradi huu amesema kua: “Mradi unajengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa (mt 1500), una vyoo (200), vimegawanyika upande wa wanaume na wanawake, vipo katika tabaka la chini, sehemu ya juu (usawa wa uso wa ardhi) imepandwa bustani pia kuna msukumo wa maji kwenye eneo lenye ukubwa wa (mt 656), kwa ajili ya kupendezesha eneo, kwani lipo katika njia inayo tumiwa na mazuwaru, hali kadhalika kuna sehemu maalumu kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum kama vile wazee na watu wenye ulemavu, jemgo hili limewekwa kila kitu kinacho hitajika, kuna hita, viyoyozi, matenki ya maji, chumba cha ukaguzi, ofisi na stoo pamoja na mtambo wa kisasa wa kutoa hewa chafu, aidha kuna sehemu ya kutawadhia na sehemu ya maji ya kunywa, na kuna sehemu ya huduma za kiafya na mfumo maalum wa taa na zima moto”.

Kumbuka kua kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu tangu kuanzishwa kwake kimesha tekeleza na kusimamia makumi ya miradi mikubwa na mamia ya miradi midogo na ya kati, ukiwemo mradi huu, ndani na nje ya Ataba tukufu, asilimia kubwa ya miradi hiyo imefanywa na wananchi wa Iraq kwa kushirikiana kati ya kitengo hiki na mashirika ya kiiraq kutoka nje ya Ataba, au baadhi ya mashirika yenye watumishi wa kigeni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: