Katika hatua ya kuratibu utendaji wa kitaasisi, kutokana na maendeleo ya dunia katika sekta hiyo, Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya maelekezo ya kiongozi wake mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi imeanza kuratibu mfumo wa utendaji kitaasisi uitwao (branding), ambao ni sehemu muhimu kwa taasisi yeyote, kupitia hiyo unaweza kuandaa utambulisho unaoweza kutumika kwa taasisi nyingine yeyote unayo taka kufanya nayo kazi, na kuandika muongozo kwa kila harakati au kazi maalum inayo fanywa na Ataba.
Kutokana na swala hili tumeongea na rais wa kamati inayo shughulikia swala hilo na mjumbe wa kamati kuu ya uongozi katika Atabatu Abbasiyya bwana Kadhim Abadah, amesema kua: “Baada ya utafiti mwingi na vikao mbalimbali pamoja na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya, leo tumeanza hatua ya kwanza ya swala hili, tumefanya kikao kikubwa na viongozi wa idara za Ataba tukufu, kwa ajili ya kuutambulisha mradi huu na malengo yake pamoja na mafanikio yatakayo patikana kutokana na utekelezwaji wake, kuanzia usanifu, machapisho na mambo mengine, na namna ya kutumia nembo rasmi ya Ataba tukufu chini ya utaratibu maalum, sambamba na kufafanua kwa kina namna ya utumiaji wake kwenye barua mbalimbali za nje na ndani, pamoja na sare maalum itakayo onyesha umoja wa shughuli za Atabatu Abbasiyya, kwa kufanya vikao nao pamoja na wajumbe wa kamati, na kujadili mambo yatakayo tekelezwa hivi karibuni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu”.
Akaongeza kua: “Hakika nembo ndio roho ya taasisi na utambulisho wake, hutumika kuwasiliana na watumishi wake pamoja na sekta za nje, kwa kupitia nembo huangaliwa malengo, ujumbe na thamani yake kibinadamu, ili tuweze kupata picha inayo wakilisha kundi kusudiwa”.