Kutoka Madaaini hadi Karbala: Watumishi wa mazaru ya Salmani Muhammadi wanampa pole Imamu Hujjat (a.f) katika kumbukumbu ya kifo cha babu yake Abu Abdillahi Hussein (a.s)

Maoni katika picha
Kama kawaida yao katika mwezi wa Muharam tena ifikapo jioni ya mwezi (21 Muharam) kila mwaka, katika malalo mbili tukufu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), watumishi wa mazaru ya swahaba mtukufu Salmani Muhammadi (r.a) kwa kushirikiana na maukibu ya Answaru bibi Ruqayyah (a.s) katika mji wa Madaaini, wamefanya kumbukumbu ya kifo cha mjukuu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake pamoja na wafuasi wake, wameomboleza yaliyojiri siku ya Ashura ambayo huonekana mapya kila mwaka, pia ni mfano mkubwa wa kujitolea na utiifu, kupitia maukibu kubwa ya kuomboleza iliyokua na waomblezaji zaidi ya (1,500).

Waombolezaji wamesimama kwa mistari iliyo shikana, uombolezaji ulianzia katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ambapo wamefanya majlis ya kuomboleza iliyo husisha usomaji wa kaswida na matam za Husseiniyya, zilizo elezea waliyo fanyiwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) katika siku kama hizi kwenye ardhi hii, kuuliwa, kunyangánywa vitu, kuchomewa mahema na mengineyo miongoni mwa jinai za kibinadamu.

Baada ya hapo waombolezaji wakaelekea kwenye malalo ya bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein (a.s) kwa ajili ya kufanya kama walivyo fanya katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), huku wakiimba kaswida na tenzi zilizo amsha hisia za huzuni kutokana na kifo cha Abu Abdillahi Hussein (a.s).

Uongozi maalum wa mazaru ya Salmani Muhammadi umezishukuru Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kwa mapokezi mazuri na ukarimu walio fanyiwa.

Kumbuka kua Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya bado zinaendelea kupokea mawakibu za waombolezaji kutoka ndani na nje ya mkoa mtukufu wa Karbala, mawakibu bado zinaendelea kuja kutokana na ratiba iliyo pangwa na kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kuanzia kumi la kwanza, la pili na la tatu katika mwezi wa Muharam, na huendelea hadi mwisho wa mwezi wa Safar.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: