Mada zinazo shindaniwa:
- 1- Adabu (Harakati za adabu na nafasi yake katika kusambaza utamaduni wa Ahlulbait (a.s) katika bara la Afrika).
- 2- Somo la Quráni katika zama hizi na upeo wa usasa katika bara la Afrika.
- 3- Hadithi tukufu na wanahadithi wa kiafrika.. juhudi na historia.
- 4- Muingiliano wa kiitikadi baina ya Dini, makundi na miji ya kiafrika.
- 5- Uhalisia wa milengo ya kidini katika bara la Afrika na mwitikio wake kwenye jamii za kiafrika.
Masharti ya shindano:
- 1- Utafiti utokane na mada zilizo tangazwa, na mtafiti abainishe mada anayo andika.
- 2- Utafiti usiwe umeshawahi kutumika kwenye shindano lingine au kuchapishwa mahala pengine.
- 3- Tafiti zitawasilishwa kwenye kamati ya majaji, na hawalazimiki kurudisha tafiti zitakazo kosa sifa ya kushiriki kwa wahusika.
- 4- Utafiti usiwe chini ya kurasa (15) wala usizidi kurasa (35) kwa ukubwa wa (sm 2.5) kila upande, na hamishi ya (sm 3.5) upande wa kulia.
- 5- Uandikwe kwa lugha ya kiarabu salama, ukubwa wa hati uwe (14), aina ya hati iwe (Traditional Arabic) na uandikwe kupitia program ya (word).
- 6- Kwenye karatasi ya juu (jalada) muandishi aandike jina la mada iliyo fanyia utafiti, jina lake kamili, sehemu anayo fanyia kazi na jina la nchi.
- 7- Mtafiti anatakiwa kuzingatia kanuni za tafiti za kielimu kwa kuangalia uhalisia wa mambo, asiandike kama hadithi ya incha, na anatakiwa kutaja vitabu rejea na majina ya waandishi wa vitabu hivyo.
- 8- Utafiti usiwe umefutwa futwa, kiwango cha ufutaji kisizidi asilimia ishirini (%20).
- 9- Kituo hakiwajibiki kurudisha tafiti kilizo pokea kwa wahusika.
- 10- Upokeaji wa tafiti umeanza (16/09/2019m) hadi (20/11/2019m) kupitia parua pepe ifuatayo: africancenter22@gmail.com
- 11- Tafiti zitaandikwa katika jarida la (Dirasaat Afriqiyya).
Kwa maelezo zaidi piga sim (07801020562).
Zawadi za washindi ni:
- Mshindi wa kwanza: $1000 dola za kimarekani.
- Mshindi wa pili: $800 dola za kimarekani.
- Mshindi wa tatu: 500 dola za kimarekani.
- Zawadi saba za wanaofuata: $100 dola za kimarekani.
- Vyeti ya ushiriki kwa wote watakao shiriki.