Katika kusaidia sekta ya kilimo: Shamba boy wa Alkafeel wana andaa mbegu bora za matunda na shirika la Aljuud latengeneza dawa

Maoni katika picha
Karbala tukufu ni miongoni mwa mikoa mashururi kwa matunda ya (Tufaha, Mishmish, Peasi na Pera), hivi karibuni miti hiyo ya matunda imeanza kushambuliwa na wadudu hatari waitwao (Capnodis tenebrionis) shamba boy wa Alkafeel kwa kushirikiana na idara ya kilimo ya mkoa wa Karbala/ kitengo cha maelekezo na mafunzo ya kilimo pamoja na kitengo cha kulinda mimea, wameandaa semina ya kuwatambulisha wakulima maradhi hayo na namna ya kupambana nayo, pamoja na kuwafundisha dawa yake ambayo inatengenezwa na shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud, dawa hiyo inatibu mimea na kuzuwia kuenea kwa maradhi hayo.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa shamba boy wa Alkafeel Ustadh Muayyad Haatif: “Semina hiyo imefanyika ndani ya ukumbi wa shamba boy wa Alkafeel, wamefundishwa hatari ya maradhi hayo na usambaaji wake na jinsi yanavyo teketeza mashamba ya miti, pamoja na umuhimu wa kushirikiana na taasisi za serikali pamoja na sekta zisizo fungamana na wizara, na kuongeza uwelewa wa baadhi ya maradhi na jinsi ya kujikinga nayo au kuyatibu, kutokana na kujali kwetu kutoa msaada japo kidogo ndio tukaandaa semina hii ambayo imehudhuriwa na wakulima mbalimbali pamoja na watafiti wa maswala haya, wameambiwa hatari za wadudu hao na kuelekezwa namna ya kupambana nao na kuwaangamiza, kwa kutumia dawa inayo tengenezwa na shirika la teknolojia ya viwanda na kilimo cha kisasa Aljuud chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaongeza kua: “Nadwa imetoa mafunzo ya nadhariya na vitendo chini ya watalamu wa teknolojia ya viwanda na kilimo cha kisasa Aljuud kupitia muwakilishi wao Mhandisi mtaalam wa kilimo ambaye amesherehesha kwa kina bidhaa zinazo tengenezwa na shirika hilo pamoja na ubora wa bidhaa hizo, kuanzia mbolea na dawa za aina tofauti zinazo weza kuangaliza maradhi ya miti hii ya matunda na mingine tena zilizo onyesha mafanikio makubwa katika majaribio mbalimbali”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: