Kitengo cha uangalizi wa kihandisi kimeanza mapema kufanya maandalizi ya Arubaini

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu wameanza maandalizi maalumu ya ziara ya Arubaini, inayo tarajiwa kuhudhuriwa na idadi kubwa ya mazuwaru, kwa ajili ya kuwapa huduma bora, kitengo kimeweka mkakati kamili na kuuwasilisha kwenye kikao cha idara zinazo husika na ujenzi.

Rais wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi Mhandisi Samiri Abbasi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Mafundi wa idara wanafanya kila wawezalo kuandaa mazingira ya kutoa huduma na kukamilisha mahitaji yote ya mazuwaru watukufu, ndani na nje ya Ataba”.

Mhandisi Muhammad Mustwafa Shaakir kiongozi wa idara ya ujenzi amesema kua: “Tumewasilisha mkakati kamili kwenye kikao kuhusu ziara, ambao tumeanza kutekeleza sehemu ya mkakati huo muda si mrefu, tumegawa majukumu kwa wahandisi na viongozi wa idara, kwa ajili ya kuhakikisha tunatoa huduma bora kwa mazuwaru watukufu”.

Akabainisha kua: “Miongoni mwa mambo tuliyo fanya ni kutengeneza vyoo (90) katika jengo la Alqami, na kukarabati vyumba vyote vya malazi katika jengo la Shekh Kuleini pamoja na kufunga feni za kunyunyiza maji katika maeneo yanayo zunguka haram, pia idara imezifanyia matengenezo baadhi ya barabara zinazo elekea haram pamoja na kukarabati shule (19) zilizopo katika mji wa Karbala kwa ajili ya kuzitumia kwa malazi ya mazuwaru”.

Akasisitiza kua: “Kazi zote tulizo kubaliana zimesha anza kutekelezwa, siku za mbele tutatangaza ukamilifu wake, kazi zote zinalenga kuwahudumia mazuwaru”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: