Miongoni mwa maandalizi ya mwaka mpya wa masomo: Shule za Al-Ameed zinafanya kikao kikubwa cha walimu na wafanyakazi wa idara zake…

Maoni katika picha
Miongoni mwa maandalizi ya kuanza mwaka mpya wa masomo (2019-2020m), uongozi wa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya Jumatatu (23 Muharam 1441h) sawa na (23 Septemba 2019m), wamefanya kikao kikubwa cha watumishi wa malezi na uwalimu wa shule za Al-Ameed, kwa ajili ya kujadili mikakati na selebasi za masomo zinazo tumika katika shule za Al-Ameed, kwa ajili ya kuweka mpango wa kuboresha elimu na huduma zingine katika shule hizo.

Mkutano huu unakusudia kuongeza maendeleo katika elimu na malezi, na umekua na faida kubwa kwa mujibu wa maelezo ya walimu walio hudhuria kwenye mkutano huo.

Kumbuka kua kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinajiandaa kuingia mwaka mpya wa masomo hivyo kinajipanga kupata matokeo bora ya masomo kama ya miaka ya nyuma.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: