Katika kuomboleza kifo cha Imamu Zainul-Aabidina (a.s): Mawakibu za kuombileza zinamiminika katika malalo mbili tukufu

Maoni katika picha
Katika mazingira ya kuhuzunisha, mawakibu za waombolezaji katika mji wa Karbala asubuhi ya Jumatano (25 Muharam 1441h) sawa na (25 Septemba 2019m) zimeanza kumiminika katika malalo mbili tukufu ya Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya kutoa pole kwa Imamu wa zama Hujjat bun Hassan (a.f) kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Imamu wa nne Zainul-Aabidina na Sayyidu Saajidiin (a.s).

Mawakibu zilianza matembezi yao katika mji mkongwe huku wamebeba bendera na kuimba kaswida za maombolezo pamoja na kupiga vifua vyao, kwenda kumpa pole mwezi wa bani Hashim kwa kufiwa na mtoto wa ndugu yake Imamu Sajjaad (a.s), baada ya kuingia katika haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuomboleza, walielekea katika malalo ya bwana wa mashahidi (a.s), kwa kupitia kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu huku wakiwa na huzuni kubwa kutokana na msiba wa Imamu Sajjaad Ali bun Hussein (a.s) uliotokea siku kama ya leo mwaka wa (94) hijiriyya.

Mawakibu hizo zilihitimisha matembezi yao ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s) na zikafanya majlis na kupiga matam pamoja na mazuwaru wote waliokuwa ndani ya haram hiyo tukufu.

Kumbuka kua siku ya (25 Muharam) alifariki dunia Ali bun Hussein Sajjaad (a.s) mwaka wa (94) Hijiriyya, siku hiyo huombolezwa na waumini wote ambao ni wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kila sehemu ya dunia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: