Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya majlis ya kuomboleza kifo cha Imamu Zainul-Abidiina (a.s)

Maoni katika picha
Kumbukumbu ya kifo cha nuru ya nne miongoni mwa nuru za Muhammadiyya Imamu Zainul-Abidiina (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlis ya kuomboleza kwa watumishi wake katika ukumbi wa utawala ndani ya haram tukufu, asubuhi ya leo Jumatano (25 Muharam 1441h) sawa na (25 Septemba 2019m), ni kawaida yake kuomboleza siku za misiba ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s).

Majlis ilifunguliwa kwa Quráni tukufu, kisha akapanda mimbari Shekh Muhsin Asadiy kutoka kitengo cha Dini akazungumza historia na uhai wa Imamu Sajjaad (a.s), akaelezea nafasi aliyo kua nayo kwa baba yake Imamu Hussein (a.s) pamoja na kazi kubwa aliyo fanya katika kuelezea mapinduzi ya Imamu Hussein na kuendeleza mwenendo wake mtukufu, aidha ameeleza juhudi aliyofanya Imamu Sajjaad (a.s) ya kupambana na fikra potofu za bani Umayya.

Majlis ilifungwa kwa kusoma kaswida na tenzi za kuomboleza zilizo onyesha namna nyoyo za wafuasi wa Ahlulbait (a.s) zinavyo umia kutokana na kifo cha Imamu Ali bun Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: