Miongoni mwa ratiba ya semina ya Quráni Aljuud ya kwanza, ambayo ni miongoni mwa program za mradi wa Quráni katika vyuo na Maahadi za Iraq, Maahadi ya Quráni tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya imefanya kisomo cha Quráni kilicho hudhuriwa na wakufunzi wengi wa semina.
Kisomo kimefanyika ndani ya harama ya Abbasi na kuhudhuriwa na wahadhiri wa vyuo wanaoshiriki kwenye semina, pamoja na jopo la wasomaji wa Quráni, kikao kilifunguliwa kwa Quráni iliyo somwa na msomaji wa Atabatu Abbasiyya bwana Mustwafa Swaraaf, kisha akasoma Ustadh Muhammad Twayyaar, halafu akasoma msomaji wa Atabatu Husseiniyya Bariri Haairiy na mwisho akasoma, msomaji wa Atabatu Abbasiyya Ammaar Alhilliy.
Tambua kua Maahadi ya Quráni tukufu tangu ilipo anzishwa imesha fanya miradi mingi, kila mmoja unalenga kundi maalum katika jamii, kwa lengo la kueneza utamaduni wa Quráni kaina ya watu.
Kumbuka kua mradi wa Quráni katika vyuo vikuu na Maahadi za Iraq ni moja ya miradi muhimu katika Atabatu Abbasiyya, na umepata mwitikio mkubwa katika miaka yote ambao umekua ukifanywa na mwaka wa mwisho ulikua na washiriki zaidi ya (2000) wanafunzi wa kiume na wakike.