Maukibu ya kuomboleza kwa pamoja: Watumishi wa Ataba mbili tukufu wanampa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kumbukumbu ya kifo cha Imamu Zainul-Abidiina (a.s)

Maoni katika picha
Kwa nyoyo zilizo jaa majonzi na simanzi baada ya Adhuhuri ya Jumatano (25 Muharam 1441h) sawa na (25 Septemba 2019m), watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wamefanya matembezi ya pamoja kwa ajili ya kumpa pole bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Imamu Zainul-Abidiina (a.s).

Matembezi yalianzia ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), walisimama kwa mistari kisha wakaelekea kwenye malalo ya bwana wa mashahidi (a.s), kwa kupitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili huku wakiimba kaswida za kuomboleza msiba waliopata watu wa nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), walipo wasili kwenye malalo ya bwana wa watu hufu (Abul-Ahraar) wakapokelewa na ndugu zao watumishi wa Atabatu Husseiniyya na wakaendelea kuomboleza kwa pamoja, halafu wakafanya majlis na kupiga matam huku mazuwaru waliokuwepo nadi ya haram hiyo wakishiriki pamoja nao.

Fahamu kua mawakibu za kuomboleza katika mji wa Karbala zilianza kumiminika katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya tangu asubuhi ya leo, kwa ajili ya kumpa pole Imamu wa Zama Hujjat bun Hassan (a.f), kutokana na kifo cha Imamu wa nne Zainul-Abidiina na Sayyidu Sajidiin (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: